siku ya Jumatano tarehe 18/10/2023 Mhe. Fatma Mohammed Rajab Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasilisha Hati za Utambulisho  kwa Muadham Sultan Haitham Bin Tariq wa Oman  katika katika kasri la Al Baraka. Wakati wa mazungumzo Muadham Sultan Haitham ameshukuru  kwa uhusiano mzuri uliopo wa Kihistoria na kindugu  baina ya Oman na Tanzania na kuahidi kuendeleza  ushirikiano  huo katika maeneo ya kijamii na kiuchumi. Mhe. Balozi Fatma Rajab alishukuru kwa kuweza kuwasilisha  Hati zake kwa kipindi kifupi na kuahidi  ataendeleza  na kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kwa maslahi ya pande zote mbili. Vilevile, Mheshimiwa Balozi pia aliishukuru Serikali ya Oman kwa misaada yake ya Kimaendeleo hasa katika utekelezaji wa ahadi za Marehemu Sultan Qaboos ikiwemo ujenzi wa Kituo Cha Afya cha  Mahonda Zanzibar,  ukarabati wa jengo la Makumbusho la Beit Al Ajaib, na Uchimbaji wa Visima 100 Tanzania Bara.