Mheshimiwa Dr. Tax Stegomena, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na Mwenyeji wake Mheshimiwa Sayyid Badr Al Busaidi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman
Mheshimiwa Dr. Tax Stegomena, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya ziara ya kikazi nchini Oman tarehe 10 hadi 12 December 2022. Akiwa ziarani nchini Oman alikutana na Mwenyeji wake Mheshimiwa Sayyid Badr Al Busaidi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman. Katika mazungumzo yao walieleza kuridhika na kuimarika kwa uhusiano baina ya Tanzania na Oman na kueleza ipo haja ya kuongeza jitihada za makusudi katika kuimarisha uhusiono katika uchumi, biashara na Uwekezaji. Walikubaliana kuwa maeneo yaliyokubaliwa katika kikao cha tume ya pamoja ya ushirikiano ni maeneo ya vipaumbele baina ya Tanzania na Oman. Vilevile Mheshimiwa Stegomena Tax alihudhuria kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Oman na Tanzania na kusaini taarifa ya pamoja ya Mambo yaliyokubaliwa katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Oman. Kikao cha tume ya Pamoja kiliazimia kushirikiana katika masuala ya Ushirikiano jstika Biashara, viwanda, uwekezaji, kilimo na mifugo, uchumi wa Buluu, mawasiliano, uchukuzi na Tehama, Masuala ya Kazi na Ajira, Nishati na Mafuta, zimamoto na uokoaji, uhamiaji , utalii na uhifadhi wa kumbukumbu, nyaraka na malikale. Katika ujumbe wake aliiongozana na Mhe Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Nishati, Professor Jamal Katundu, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, ajira , vijana na wenye Ulemavu, Balozi Fatma Muhammed Rajabu Naibu katibu mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mheshimiwa Waziri alipata wasaa wakutembelea Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na TEHAMA ambapo Wiziri wa Oman alieza nia ya Serikali ya Oman kushitikiana na Tanzania katika maeneo ya Bandari, Maeneo huru ya Biashara, usafirishaji wa Majini pamoja na Serikali mtandao, mkongo wa Mawasiliano, Matumizi ya Satellite katika sekta ya TEHAMA. Pia walitembelea Wizara ya Biashara Viwanda na Uwekezaji ambapo mazungumzo yalijikita katika kuimarisha Biashara, uwekezaji, na viwanda. Mheshimiwa Waziri pia alitembelea Mamlaka ya Uwekezaji Oman, Makumbusho ya Tafa na Opera House ya Oman pamoja na ofisi za Ubalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo walipokelea na mwenyeji wao Mheshimiwa Abdalah Abasi Kilima, Balozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman.