TAARIFA MUHIMU KWA WATANZANIA WAISHIO OMAN
KUKAMILIKA KWA MFUMO WA UPOKEAJI WA MAOMBI YA PASSPORT MPYA ZA KIELEKTRONIKI UBALOZINI
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN UNAWATANGAZIA KUWA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA IMEKAMILISHA UWEKAJI MFUMO UNAOWEZESHA WATANZANIA KUOMBA PASSPORT MPYA ZA KIELEKTRONIKI HAPA UBALOZINI. KUKAMILIKA KWA HATUA HII KUNAWEZESHA WATANZANIA WALIOPO HAPA OMAN KUWASILISHA FOMU ZAO ZA MAOMBI YA PASSPORT MPYA ZA KIELEKTRONIK HAPA UBALOZINI KWA UTARATIBU ULIOPANGWA
CHINI YA UTARATIBU HUU, MUOMBAJI AMBAYE AMEISHAJAZA FOMU MTANDAONI, AKALIPIA DOLA 15 NA KUCHAPISHA FOMU YAKE ATATAKIWA KUOMBA MIADI KWA KUPIGA SIMU AU KUTUMA BARUA PEPE UBALOZINI ILI KUPANGIWA MIADI YA AJE LINI NA KWA MUDA GANI ILI KUKABIDHI FOMU ZAKE KWA AFISA WA PASIPOTI UBALOZINI
AFISA ATAPOKEA FOMU NA KUHAKIKI USAHIHI WA TAARIFA KWA MUJIBU WA NYARAKA ZILIZOAMBATANISHWA NA BAADA YA KURIDHIKA NA HALI YA OMBI NA VIAMBATANISHO HUSIKA ATAMPATIA ANKARA YA KULIPIA DOLA 75 ZILIZIZO BAKIA
BAADA YA KUPATA ANKARA MUOMBAJI ATATAKIWA KUINGIA KWENYE MTANDAO WA MALIPO YA SERIKALI www.epay.gepg.go.tz NA KUFUATA MAELEKEZO. MALIPO YATAKUWA TAYARI NDANI YA MASAA 24 SIKU ZA KAZI TANGU MALIPO YALIVYOFANYIKA
BAADA YA MALIPO KUKAMILIKA MUOMBAJI ATAPIGA SIMU TENA KWA AJILI YA KUPANGIWA MIADI YA KUJA KUPIGA PICHA, KUCHUKULIWA ALAMA ZA VIDOLE NA KUSAINI
NAMBA YA KUPIGA KUOMBA MIADI NI +96871703943 NAMBA HII NI MAALUM KWA KUOMBA MIADI NA ITAKUWA WAZI KUANZIA SAA 3 (09.00AM) HADI SAA 8 (2PM JUMAPILI HADI ALHAMIS) NA ANUANI YA BARUA PEPE NI tamuscat@omantel.net.om
ZINGATIA YEYOTE ATAKAEKUJA BILA MIADI HATOHUDUMIWA NA ATATAKIWA KUFUATA UTARATIBU WA KUOMBA MIADI
MNAKUMBUSHA KUWA PASIPOTI ZA SASA ZITAKOMA KUTUMIKA IFIKAPO JANUARI31. 2020. OMBA PASIPOTI MPYA SASA USISUBIRI DAKIKA ZA MWISHO
IMETOLEWA NA :
UBALOZI WA TANZANIA. MUSCAT, OMAN
16 JULY 2019