Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akizungumza  na Mabalozi wanao kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali (hawapo pichani), mazungumzo hayo yalifanyika leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Mhe. Mahiga alitumia fursa hiyo kuwasisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kikamilifu, sambamba na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

  • Waheshimiwa Mabalozi wakimsikiliza Waziri Mahiga, kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Grace Mgovano na Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Matilda Masuka.
  • Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi wakimsikiliza Waziri Mahiga. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Haji, Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Omar Mzee.
  • Mazungumzo yakiendelea.
  • Picha ya pamoja Mhe. Waziri na Waheshimiwa Mabalozi