ZIARA RASMI NCHINI OMAN YA MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JUNI 12-14-2022.

 

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na mwenyeji wake Mtukufu Sultan Haitham bin Tarik, Sultan wa Oman.

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alifanya ziara rasmi nchini Oman kuanzia tarehe 12 June hadi 14 June 2022 kwa mwaliko wa Mtukufu Sultan Haitham bin Tarik. Alipowasili uwanja wa ndege alipokelewa na Mwenyeji wake na kuelekea Kasri ya Al Alam ambako baada ya kuwasili yalifanyika mapokezi Rasmi kupokea heshima ya Mizinga 21, Mapokezi yalifuatiwa na mazungumzo rasmi kati ya Mheshimiwa Rais na Mtukufu Sultan ambayo yalihudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka serikali za Oman na Tanzania. Katika mazungumzo yao viongozi hao walielekeza umuhimu wa kuongeza juhudi za kukuza biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Oman na kuwa kiwango cha sasa hakiridhishi na hakiakisi uhusiano wa kindugu uliopo baina ya nchi zetu. 

Katika ziara hii Mheshimiwa Rais alishiriki katika matukio mbalimbali ikiwemo kutembelea makumbusho ya Taifa ya Oman na kujionea utajiri wa historia ya Oman lakini pia historia ya Oman na Zanzibar. 

 Mheshimiwa Rais alitembelea kituo cha Dar Al Hanan, ambacho kinatoa malazi kwa familia zinazoleta watoto wao kupata matibabu ya kansa mjini muscat, kituo hiki kinaendeshwa na Taasisi ya Oman Cancer Association, ambayo ilianzisha utaratibu huu kuwasaidia wanaotoka nje ya Muscat wasipate shida ya malazi na kukwepa kuwaleta watoto kwenye matibabu.

Mheshimiwa Rais (katika picha) alipotembelea kituo cha Dar Al Hanan kinachosimamiwa na kuendeshwa na Taasisi ya Oman Cancer Association.

Mheshimiwa Rais pia alihutubia Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Oman na kueleza kuwa Tanzania iko tayari kupokea wawekezaji na kukuza biashara baina ya Tanzania na Oman kufuatia jitihada za makusudi zilizofanywa ba Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wake ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara. 

Mheshimiwa Rais pia alishuhudia utiwaji saini wa mikataba kadhaa baina ta Serikali ya Oman na Tanzania, na pia Taasisi za serikali pamoja na sekta binafsi. Mikataba iliyosainiwa kwa upande wa Serikali ni 

 

Agreement on Cooperation in Oil and Gas sector, Agreement in Cooperation in Tourism and Natural Resources, Agreement in Cooperation in Higher Education na Agreement on Cooperation Between National Museum of Tanzania and National Museum of Tanzania. 

Kwa Upande wa sekta binafsi mikataba iliyosainiwa ni, Mkataba wa ushirikiano baina ya vyama vya wafanya biashara wa Tanzania na Oman (Oman Chamber of Commerce na Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture), Makubaliano ya maelewano kati ya Shirika la Ranchi za Taifa, Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Kampuni ya Viwanja vya ndege ya Oman na Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KADCO) na makubaliano ya Maelewano baina ya Mamlaka ya maghala ya chakula ya Oman na Jumuiya ya wauzaji mbogamboga na matunda (TAHA)

Mheshimiwa Rais akishuhudia utiwaji Saini wa ushirkiano baina ya wizara ya Utalii ya Taifa ya Oman na Tanzania. Mikataba hiyo ili sainiwa na Mhe. Balozi Pindi Chana (Waziri wa Maliasiri na Utalii) na Mh. Salim bin Mohammed Al Mahrouqi (Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Oman)

 

 

Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Januari Makamba akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe. Sayyid Badar Bin Al Busaidi baada ya kutiwa saini Makubaliano ya Ushirkiano sekta ya Nishati 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar Investment Promotion Authority (ZIPA) Ndugu Sharif A. Sharif na Mhe. Sultan Salim Saeed Al Habsi  Oman Investment Authority (OIA) wakitia Saini makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili mbele ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

 

 

(Pichani Juu) Mkusanyiko wa picha ukionesha  Mheshimiwa Rais akishuhudia kusainiwa kwa mikataba mbali mbali baina ya Mawaziri na viongozi wa sekta binafsi wa Oman na Tanzania katika hotel ya Al Bustan Palace, Muscat Oman.

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Pindi Chana akibadilishana hati za makubaliano ya ushirkiano sekta ya Makumbusho ya Taifa na Mambo ya Kale wa Oman Mhe Jamal Bin Hassan Al-Moosawi, Katibu mkuu wa Makumbusho ya Taifa.

Vilevile, Mheshimiwa Rais  alipata fursa ya kukutana na wana diaspora wa Tanzania wanaoishi nchini Oman, mkutano huu ulihudhuriwa na washiriki wanaofikia 500 miongoni mwao wakiwa ni Watanzania wanaofanya shughuli mbalimbali nchini Oman na kundi la pili ni Waoman wenye asili ya Tanzania

                Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akihutubia kongamano la Watanzania waishio nchini Oman

 

Umoja wa Wana Diaspora ya Tanzania nchini Oman uliwasilisha risala kwa mheshimiwa Rais. Katika risala yao walimpongeza Mheshimiwa Rais kwa hatua anazochukua kuifungua nchi na kushawishi wafanya biashara wa Oman kuwekeza na kufanya biashara Tanzania. Pamoja na pongezi hizi walieleza changamoto zinazowakabili na mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto hizo. 

 

Picha Juu: Wana Diaspora waliohudhuria mkutano 

Mheshimiwa aliwaeleza kuwa amepokewa kwa heshima kubwa inayothibitisha uhusiano wa kindugu uliopo baina ya Tanzania na Oman, aliwaasa kuwa watulivu na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu pamoja na kuheshimu mila na desturi za mahala wanapoishi

Katika maswali na majibu, wana diaspora walionyesha kuhitaji kuwepo kwa mfumo wa hifadhi ya jamii utakaowawezesha kujiwekea akiba ya uzeeni ili watakapofikia umri wa kustaafu wasihangaike, pia walieleza haja ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Kufanya Safari za Kuja Oman kwa kuzingatia soko kubwa na la uhakika la abiria na mizigo pamoja na Benki za Tanzania kufungua matawi yake nchini Oman ili kuwawezesha wanadiaspora kuweka na kusafirisha fedha zao nchini Tanzania kwa urahisi.