Balozi mpya wa Tanzania nchini Oman, Maulidah Hassan amewasili jijini Muscat kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake ya kidiplomasia.

Balozi Maulidah alipokelewa na maafisa waandamizi wa Serikali ya Oman wakiongozwa na Naibu Mkuu wa Itifaki pamoja na mabalozi na manaibu mabalozi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Algeria, Morocco, Senegal na Kenya.

Pia alipokelewa na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman wakiongozwa na Mustafa Ussi.